Tuesday, 8 December 2015

Safari ya Hip-Hop

Safari hii wameamua kupumbaza kwa staili ya aina yake, wanakuja kidizain, mmoja mmoja waki wekeza na kuchota kwa kuchota. walianzia juu wakafika mpaka south africa sasa hivi wana panda taratibu huku waki malizia, .. Mugabe kawatimua sisi ndio tuna wakaribisha, wanyonyaji wafisadi, wamevaa ngozi ya kondoo {weupe} lakini roo zao zinakiu ya kubeba na kuji limbikizia.

Hebu cheki mererani na kwenye machimbo mengine utaamini kuwa wanakuja mmoja mmoja ila kama mililioni moja, wana chota kwa kusomba, mamashine makubwa yenye uwezo wa kufyonza hazina ya kizazi chetu kwa sekunde na kutuacha watupu, walianza kuipumbaza serikali sasa hivi mpaka vyumbani wanaingia , eti mavoluntia!!! nani kasema kunamtu asio taka kulipwa maishani? hivyo ni viji staili tu vya kidizain... kifupi wanakuja kuchota hata ujuzi na nafasi zetu za kazi kwenye future.

haya mi yangu macho tuu! sijui kama kizazi cha mwafrica kitapata nafasi ya kuiongoza dunia , zaidi ya kuendelea kuwa wa kwanza kwenye listi ya masikini wa dunia,

Ndoto zangu za zam ya mwafrica kuiongoza Dunia zime anza kufifia
haswa kwajinsi tulivyo hatuna hisia, ...

Iweje Mugabe awafukuze sisi tuwakaribishe?

Bida
Mzee wa Hisia kali za Chaka asilia